Popular Posts

Monday, 6 May 2013

WADAU WOTE WA ELIMU KANDA YA KATI WAHAMASISHWA KUCHANGIA ELIMU

Wale wakazi wa kanda ya kati Nchini Tanzania hususani mikoa ya Dodoma na Singida wanaombwa kutoa ushirikiano wa hali na mali katika kutoa elimu na kuhamasisha katika masuala mbalimbali. Kikundi cha vijana waliopata elimu na wale wenye mwamko wamekubaliana kuanzisha Foundation iitwayo SANZA EDUCATION FOUNDATION (SEF) kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali yahusuyo elimu. Masuala yanayozungumziwa ni pamoja na:-
1. Kushawishi, kushauri wazazi, viongozi wa serikali na tasaasisi mbalimbali ikiwemno za dini na walimu ili kuwajengea wanafunzi uwezo mzuri kitaaluma
2.kuchangia na kutoa misaada ya hali na mali ili kuwawezesha watoto wasio na uwezo wa kifedha ili waweze kupata taaluma
3.kuongea na wanafunzi wa ngazi mbalimbali kuanzia shule za msingi, shule za sekondari, vyuo mbalimbali wale wa elimu ya juu.
4. kutoa elimu juu ya umuhimu wa elimu katika jamii
5.kwa mawasiliano zaidi na ushauri unaweza kutoa maoni kupitia email address sanzasef@yahoo.com 

BAADHI YA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI WAKIWA SHULE HUKO MANYONI SINGIDA

No comments:

Post a Comment