Wamachinga wanadai kule waliko hamishiwa hamna biashara, wateja wala miundo mbinu yoyote kiasi kwamba mitaji inakata. so wameamua kurudi eneo la stand hadi hapo serikali itakapo wajengea miundo mbinu na soko kulihamishia huko. Mch. Msigwa yupo nao sasa hivi polisi wanamtafuta. amesema hadi kieleweke. machinga wanamlinda kama rais kiasi kwamba polisi pamoja na kuziba njia zote/kumzunguka hadi sasa hajakamatwa. Muda si mrefu ataongea na vyombo vya habari. wamachinga wamesema wawamalize kwanza ndo wamshikw. mia
Nimesikia radio maria muda sio mrefu,wanasema police wanawamwagia maji ya kuwasha hata wazee na watoto waliotoka kanisani.Najua hapo yupo kamuhanda hakuna busara itakayotumika,ukizingatia majuzi alisifiwa bungeni na lukuvi kwa 'kazi'nzuri anayoifanya.
Vurugu zinaendelea hapa mjini baina wa wamachinga na polisi wa kuzuia fujo (FFU). Wakati Mbunge (Mch Msigwa) ameruhusu wamachinga na wauza mitumba waendee na biashara zao, Meya wa Manispaa amezuia. Hali ni tete.FUATILIA MATUKIO KATIKA PICHA
WAMACHINGA WAKISUKUMA GARI LA MBUNGE MH.PETER MSIGWA

No comments:
Post a Comment