Kutokana na barua yenye Kumb Na CAC.205/228/01/C/14 ya
tarehe 2 Julai,2013, Kutoka Menejiment ya utumishi wa umma, inayohusu
kupandisha mshahara kwa watumishi wa serikali yenye kichwa cha habari “WARAKA
WA WATUMISHI WA SERIKALI NA. 1 WA MWAKA 2013, MAREEKEBISHO YA MISHAHARA KWA
WATUMISHI WA SERIKALI” Inasema Serikali inaendelea kutekeleza sera ya malipo ya
mishahara na motisha katika utumishi wa umma mwaka 2010. Katika hatua za
kutimiza malengo ya sera hii, serikali inafanya marekebisho ya mishahara ya
watumishi wake kuanzia tarehe 1 julai, 2013. Kutokana na marekebishi hayo kima
cha chini kitakuwa kutoka 170,000/= hadi tsh 240,000/= kwa mwezi. Mishahara ya
watumishi wengine imeongezwa kwa wastani wa 8.41% . imesainiwa na KATIBU MKUU (UTUMISHI
G.D.Yambeshi)(Mwisho wa kunukuu).
Barua hiyo
ambayo inaonekana kuwa mwiba kwa watumishi wa kada ya UALIMU ambao walidhani
serikali itajibu madai yao ya nyongeza ya mishahara, subira hiyo haijazaa
matumaini kwani kwa mujibu wa waraka huo kada ya ualimu inaonekana iko nyuma ya
kada za afya na kilimo. Hii ni sehemu ya waraka huo ukianisha madaraja ya
mishahara mipya kuanzia julai 1, 2013.(N:B Kwa wale wasiojua ngazi ya mshahara
ya B ni ya mwenye cheti (certificate), C= Diploma, D= Degree)
WALIMU
TGTS B1= 344,000/=
TGTS C1= 432,500/=
TGTS D1= 589,000/=
TGTS E= 769,000/=
TGTS F= 1,003,000/=
TGTS G= 1,320,000/=
Wakati kwa kada ya KILIMO mambo ni mazuri kabisa kama
ifuatavyo
B= 1,060,000/=
C=1,252,000/=
D= 1,473,000/=
E=1,736,000/=
POLENI SANA WALIMU KWA KUENDELEA KUNYONYWA HAKI ZENU.
Katika waraka huu sehemu ya mwisho unasema
WARAKA HUU NI KUMBUKUMBU NA TAARIFA YA SERIKALI NA
HAIRUHUSIWI KUTANGAZWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI
Naamini kilio cha wafanyakazi mungu atakijibu siku moja ,tumechoshwa na ahadi za uongo na ukandamizaji uliopo Tanzania ya sasa.Nini kinazuia mishahara kupandishwa.Tunaona wazi gesi inayovunwa, madini yanayochimbuliwa, utalii na kodi mbali mbali. Serikali inashindwa kutambua ongezeko la ugumu wa maisha, thamani ya fedha ilivyoporomoka ,wafanyakazi shime tuungane kukomboa ukandamizaji huu
ReplyDelete.