WAZIRI KAWAMBWA NA WATENDAJI WA BARAZA LA MITIANI WANAPASWA KUJIUZULU NA KUCHUKUKULIWA HATUA ZA KISHERIA
Tume
ya waziri mkuu imetoa ripoti yake ya awali kuhusu sakata la kufeli vibaya
kwa wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012. Taarifa
hiyo inabaanisha kuwa moja ya sababu za maafa ya kufeli kupindukia kwa
wanafunzi wa mwaka jana ni kutumika kwa alama mpya tofauti na miaka ya
nyuma bila hata taarifa kwa wanafunzi waalimu na hata wazazi huku
mabadiliko hayo yakiwa ni siri ya baraza la mitiani na wizara ya elimu ambayo
kimsingi ndio inasimamia masuala ya kisera ya elimu nchini.
BAVICHA
inaona, japo ni taarifa ya awali, kilichosomwa bungeni ni muendelezo wa siasa
na mzaa kwa watanzania kunakofanywa na serikali ya CCM kwenye mambo nyeti ya
maisha ya watu. Kwamba
viwango vipya vya madaraja viliwekwa na Baraza la mitiani bila kushirikisha
wadau ni kiashiria cha uzembe uliokithiri wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi ambaye ndiye msimamizi wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA) na ambae
alipaswa kuhakikisha taarifa hizo ambazo ni za kisera zinafika kwa walengwa.K
Kama
Baraza lilifanya maamuzi hayo bila waziri kujua nako kunaashiria uzembe
uliobobea wa waziri huyu wa kushindwa kujua kinachofanyika na taasisi zilizo
chini yake na kwa maana hiyo ni mzigo kwa taifa na BAVICHA inasisitiza
waziri Kawambwa na wasaidizi wake wajiuzulu nyadhifa zao ili kupisha watu wenye
uwezo wa kusimamia sekta hii na taasisi zilizo chini yake.
Pia
kwa kuwa ripoti hiyo inaonyesha kuwa viwango vipya vya madaraja vilitumika pasi
walengwa kuhusishwa na kwamba tayari malaki ya vijana wameathirika kwa uzembe
huu ambapo wengine wamepoteza maisha kwa kujinyonga, ni wazi kua watendaji wa
Baraza la Mitiani la Taifa wanapaswa kuchukuliwa hatua za haraka kwa kuondoshwa
kwenye nafasi hizo sambamba na waziri anayewasimamia kujiuzulu. Licha
ya kufukuzwa mara moja kwenye nafazi zao, BAVICHA inataka sasa, kutokana na
ripoti hii, Waziri na Watendaji wa NECTA wachukuliwe hatua za kisheria kwa
kusababisha mauaji ya vijana 3 waliojinyonga kutokana na matokeo mabovu kwa
uzembe uliokithiri.
BAVICHA
inakumbusha kuwa kurudiwa kupangwa kwa matokeo ya kidato cha nne sio tiba ya
kufeli kwa wanafunzi bali ni lazima sanaa za kisiasa zinazochezwa na serikali
ya CCM kwa kuwa imeacha kushukua hatua ngumu za wahusika waliosababisha aibu
hii na pia kushughulikia matatizo ya msingi ya sekta ya elimu ili kuboresha
ubora wake.
BAVICHA
tunasisitiza kuwa ubovu wa matokeo ya mwaka jana ni kilele cha kudharauliwa kwa
walimu wa nchi hii na serikali ya CCM, mazingira mabovu ya kutolea elimu ambapo
zipo shule zisizofanana na shule, idara ya ukaguzi wa shule kushindwa kufanya
kazi yake kutokana na kutokuwa na meno na mfumo mbovu usiokidhi mahitaji
ya sasa ya taifa na dunia.
Imetolewa
leo tarehe 4.5.2013 jijini Dar es salaam na;
Deogratias
Munishi
Katibu
Mkuu –BAVICHA
+255715
887712
No comments:
Post a Comment