Popular Posts

Wednesday, 22 May 2013

VURUGU KUBWA MTWARA KUHUSU GESI HADI BUNGE LAAHIRISHWA




Habari zilizo tufikia ni kuwa zaidi ya watu nane (8) wamepoteza maisha, polis zaidi ya wanne na raia zaidi ya wanne.

Jengo moja ambalo linadaiwa kumilikuwa na CCM limechomwa moto katika eneo la Majengo na daraja linalounganisha Lindi na Mtwara limevunjwa.

Mbali na hayo pia nyumba ya mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) imechomwa moto. Katika Mji wa Mtwara milio ya mabomu na risasi ndio inayosikika kila kona. Jeshi la Polisi linajaribu kuwadhibiti vijana na watu wengine ambao wanafanya vurugu hizo.

HALI NI TETE... STAY TUNED...

Monday, 20 May 2013

BUNGE LAAHIRISHWA GHAFLA BAADA YA KAMBI YA UPINZANI KUDAI SERIKALI INAUA WAANDISHI WA HABARI

Sugu anaendelea kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani, analaumu serikali kuwa inawakandamiza waandishi wa habari anazungumzia ugaidi na utekaji na utesaji. 

Hutuba ya Sugu bungeni yasimamishwa, Bunge laahirishwa ghafula mpaka jioni, kamati ya uongozi yakutana kuijadiri ni baada ya Zambi kuomba muongozo akidai hotuba ya sugu imejaa uchochezi na uongo wa kuisema vibaya serikali ya ccm. 

Bunge limeahirishwa baada ya kambi upinzani kudai kwamba serikali inatoa kucha, macho, meno na kuwaua waandishi wa habari

USHAURI WA MH. MSIGWA ULISINGEPUUZWA VURUGU ZA IRINGA ZISINGETOKEA



Wiki iliyopita Mh. Peter Msigwa aliongelea tatizo la Wamachinga wa Iringa.



Alishauri yafuatayo:



1. Serikali ifanye mpango wa kuongea na wamachinga na kupata suluhisho la pamoja. Anasema kuwa Mwanza, Mbeya na Moshi wakuu wa Mikoa walikuwa tayari kuongea na wamachinga wa huko na tatizo lao likatatatuliwa.

2. Alionya juu ya kutumia nguvu za polisi kama suluhisho la suala hili, kwa kuwa hawa ni wananchi wenye shida inayohitaji kutatuliwa, hivyo ni busara wasikilizwe kuliko kutishwa na kuletewa polisi.

3. Alionya kuwa Polisi wanapotumika kuzuia sauti za wamachinga, wanatengeneza mazingira ya wananchi kuchukia serikali yao na kuona inawakandamiza.

Angalia zaidi video hii, BOFYA HAPA CHINI



MCHANGO WA MH. PETER MSIGWA BUNGENI

M4C YAIVUNJA CCM KATIKA JIMBO LA MH. LOWASA (MONDULI), MAMIA WACHUKUA KADI CHA CHADEMA

Godbless Lema akiwakabidhi kadi za CHADEMA wananchi wa Monduli katika kata ya Makuyuni  kwenye uzinduzi wa kampeni za udiwani. Mamia wamehama CCM na kujiunga na CHADEMA. Hili ni pigo kwa CCM kwani maeneo haya ndiyo ilikuwa ngome yake.

Mawaziri watatu kung’olewa , Baada ya kukataliwa na Wabunge Vyama Vyote (Ikiwemo wa CCM)

WABUNGE CCM WAWAKATAA

UPEPO mbaya ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) unazidi kuvuma, safari hii wabunge wake wakimtaka Rais Jakaya Kikwete kuwafukuza kazi mawaziri watatu. Mawaziri wanaotakiwa kung’olewa ni Dk. Shukuru Kawambwa (Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Dk. Mathayo David Mathayo (Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi) na Dk. Fenella Mukangara (Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo). Kama Rais Kikwete atakubali kuwaondoa madarakani mawaziri hao, hii itakuwa mara ya pili kwake kufanya hivyo. Mara ya kwanza ilikuwa Mei mwaka jana. Mwaka jana Rais Kikwete aliamua kuwaengua madarakani baadhi ya mawaziri waliokuwa wakiandamwa kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo uwajibikaji mbovu.

Miongoni mwa walioenguliwa mwaka jana ni Dk. Haji Mponda aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mustafa Mkulo (Waziri wa Fedha), William Ngeleja (Nishati na Madini na Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii). Msimamo huo wa wabunge wameutoa jana katika kikao baina yao na Rais Kikwete kilichokuwa kikitathimini mwenendo wa chama na utendaji wa wabunge. Chanzo chetu ndani ya kikao hicho kilieleza kuwa baada ya Rais Kikwete kutoa hotuba ya ufunguzi, baadhi ya wabunge walianza kuchangia, huku wengine wakishutumiana kwa kuvujisha siri za vikao nje kwa waandishi wa habari. Wabunge hao walidai kuwa mawaziri hao watatu wamekuwa mzigo kwa Serikali ya CCM kutokana na utendaji wao kutokuwa wa kuridhisha.

Walisema matunda ya uwepo wa mawaziri hao kwenye wizara husika hayaonekeni, hivyo kumtaka Rais Kikwete awang’oe. Waziri Kawambwa analaumiwa kwa kuzembea kwenye sekta ya elimu ambayo inazidi kushuka kiasi cha kuifanya serikali ifute matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana. Walisema kufutwa kwa matokeo hayo ambayo asilimia 60 ya waliofanya mtihani walipata daraja sifuri, kunadhihirisha uwezo mdogo wa Dk. Kawambwa. Wakati Kawambwa akibanwa kwa hilo, wenzake Mathayo na Mukangara wanadaiwa kuwepo wizarani bila kuonesha ufanisi wowote.Wabunge hao walidai kuwa Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi anayoiongoza Dk. Mathayo ni nyeti na ilipaswa kuwa ya pili katika kuchangia pato la taifa baada ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Walimshambulia Dk. Mathayo kuwa mzigo kwa wizara hiyo kwani alipokuwepo Dk. Magufuli (Waziri wa Ujenzi) ilikuwa ikifanya vizuri tofauti na hivi sasa. “Tusioneane aibu, huyu Mathayo ameshindwa kazi, mwenyekiti muondoe kabla mambo hayajazidi kuwa mabaya,” alisema mbunge mmoja.

JK abariki mchakato wa urais

Mapema katika hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho, Rais Kikwete aliruhusu makundi ya wana-CCM wanaotaka kuwania urais 2015 kuendelea na mchakato wa kuweka mikakati yao ya kampeni bila chuki. Kwa mujibu wa chanzo chetu katika kikao hicho ambacho waandishi hawakuruhusiwa kuingia, lengo kubwa lilikuwa ni kujadili masuala mbalimbali ya kitaifa ikiwemo utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika majimbo ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na ahadi za rais. Rais Kikwete aliwataka wana-CCM wenye nia ya kugombea urais kuendelea na mikakati yao kwa ustaarabu na kuepusha uadui kutokana na wapambe wao kuwa na kambi zaidi ya moja.

“Tuangalie makundi ya urais 2015 yasishambuliane kwa kuvunja chama, wenye nia hiyo ya kugombea waendelee na mikakati yao na si kujenga chuki kwa makundi mengine. “Mkumbuke kuwa kambi hizo za urais zinatakiwa kujitizama na wafuasi wao maana wafuasi wengi si wa kuaminika,” alisema Kikwete. Rais Kikwete aliwafananisha baadhi ya wapambe na matango pori yanayoota popote, ambapo alisema wamekuwa na tabia ya kutoa maneno huku na kupeleka upande wa pili. Tanzania Daima ilidokezwa kuwa Kikwete alikuwa na ajenda nne ambazo ni urais 2015, kuwahimiza wabunge kutembelea majimbo yao ya uchaguzi, kurudi majimboni kwao kusimamia ahadi zao, chama na zile za viongozi wa kitaifa akiwemo yeye na kuisimamia serikali na kuikosoa bila kuibomoa.

Kwamba Kikwete aliwataka wabunge hao kutumia kauli za staha wanapoikosoa serikali kama ambavyo baadhi wamekuwa wakifanya. “Mnatakiwa kuisimamia serikali na kuikosoa bila kuibomoa, lakini kuna baadhi yenu mmekuwa mnaibomoa serikali kwa jinsi mnavyochangia huko bungeni, hilo si jambo jema hata kidogo, waachieni wale wenzenu,” alisema. Katika hilo, wabunge walionya tabia ya baadhi ya mawaziri wanavyohusiana na wabunge na wanavyoonekana kwa wananchi, lakini wakaitaka serikali kutimiza wajibu wake ipasavyo kwa kutoa fedha za bajeti kama zinavyopitishwa na Bunge.

Pia ubadhirifu unaofanywa kwenye halmashauri nchini, utendaji mbovu wa baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa nchini, hivyo wakamtaka rais kukunjua makucha yake kuondokana na uozo huo.
Kuhusu kutembelea majimbo, rais alisema kuwa baadhi ya wabunge wameyatelekeza kwa kutorudi kusikiliza kero za wananchi na kutimiza ahadi zao. Aliwaonya kuwa kwa tabia hiyo wala wasije kuwaonea donge wale wanachama wengine watakaochaguliwa kuwa wabunge badala yao.

Lugola, Filikunjombe, Mpina wakaangwa

Baada ya mapumziko ya mchana, kikao hicho kiliendelea kwa wabunge kutoa madukuduku yao ambapo chanzo chetu kinasema kuwa wabunge watatu walishambuliwa kwa tabia yao ya kuikosoa serikali kwa kauli nzito. Wabunge hao ni Kangi Lugola (Mwibara), Deo Filikunjombe (Ludewa) na Luhaga Mpina wa Kisesa ambao hata hivyo wote hawakuhudhuria kikao hicho. Lugola amekuwa mwiba mkali wa kuwashambulia mawaziri wa serikali kutokana na utendaji wao kutoridhisha ambapo hivi karibuni wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), alitishia kuwataja mawaziri na watendaji wanojihusisha na rushwa pamoja na biashara ya dawa za kulevya.

Filikunjombe naye amekuwa akipinga kuunga mkono hoja za serikali huku akitumia maneno makali kama vile ‘serikali kuvaa miwani ya mbao’, kutokuwa sikivu na mengine kama hayo ambayo inaelezwa kuwa hata Rais Kikwete jana aliyatolea mfano.
Chanzo chetu kilieleza kuwa aliyeibua sakata hilo ni mbunge mmoja wa Tabora, akidai wenzao hao wamekuwa na tabia isiyokoma, na hivyo kupendekeza kuwa kama wanataka ni heri wakahamia upinzani kuliko kuendelea kuivua nguo Serikali ya CCM. Hadi tunakwenda mitamboni jana, kikao hicho kilikuwa kikiendelea na kwa mujibu wa ofisa mmoja wa chama, walitarajia kuwa kingemalizika usiku wa manane.

Source: Tanzani Daima (May 2013). Mawaziri watatu kung’olewa. Retrieved from Tanzania Daima

KILICHOKILI LEO MAHAKAMANI IRINGA-KESI YA MH.MSIGWA NA MACHINGA



Mh. MSIGWA akiwashuka kuelekea mahakamani chini ya ulinzi mkali wa polisi, hatua hii inafikiwa baada ya kutuhumiwa kuwa aliongoza maandamano na vurugu za machinga dhidi ya polisi

PICHA ZA MATUKIO YA VURUGU ZA MACHINGA NA POLISI-IRINGA MJINI

























Sunday, 19 May 2013

PETER MSIGWA AONGOZA MACHINGA KUFANYA BIASHARA, POLISI WAPIGA MABOMU

Wamachinga wanadai kule waliko hamishiwa hamna biashara, wateja wala miundo mbinu yoyote kiasi kwamba mitaji inakata. so wameamua kurudi eneo la stand hadi hapo serikali itakapo wajengea miundo mbinu na soko kulihamishia huko. Mch. Msigwa yupo nao sasa hivi polisi wanamtafuta. amesema hadi kieleweke. machinga wanamlinda kama rais kiasi kwamba polisi pamoja na kuziba njia zote/kumzunguka hadi sasa hajakamatwa. Muda si mrefu ataongea na vyombo vya habari. wamachinga wamesema wawamalize kwanza ndo wamshikw. mia Nimesikia radio maria muda sio mrefu,wanasema police wanawamwagia maji ya kuwasha hata wazee na watoto waliotoka kanisani.Najua hapo yupo kamuhanda hakuna busara itakayotumika,ukizingatia majuzi alisifiwa bungeni na lukuvi kwa 'kazi'nzuri anayoifanya. Vurugu zinaendelea hapa mjini baina wa wamachinga na polisi wa kuzuia fujo (FFU). Wakati Mbunge (Mch Msigwa) ameruhusu wamachinga na wauza mitumba waendee na biashara zao, Meya wa Manispaa amezuia. Hali ni tete.FUATILIA MATUKIO KATIKA PICHA









WAMACHINGA WAKISUKUMA GARI LA MBUNGE MH.PETER MSIGWA