baadhi ya picha zikionyesha moshi wa mabomu ya machozi. polisi wamelazimika kutumia nguvu ili kuwatawanya wamachinga ambao wahitaji muda wa masaa 8 tu kuanzia saa moja asubuh had saa 8 mchana kwa siku moja ya jumapili tu kwa wiki. wamachinga hao bado hawataki kutoka hapo maeneo ya mashine tatu iringa mjini. tukio hilo linatokea baada ya siku chache mh mchungaji msigwa alipowaruhusu wamachinga kuendelea na biashara hiyo. kwa taarifa zaidi fuatilia blog hii(picha na agustino alpha)
Popular Posts
-
Kutokana na barua yenye Kumb Na CAC.205/228/01/C/14 ya tarehe 2 Julai,2013, Kutoka Menejiment ya utumishi wa umma, inayohusu kupandisha...
-
Tamko hili limetolewa leo tarehe 3 august 2013, mkoani mbeya katika ukumbi wa royal zambezi KIKAO CHA WALIMU WA MKOA WA MBEYA CHA KUJAD...
-
Wamachinga wanadai kule waliko hamishiwa hamna biashara, wateja wala miundo mbinu yoyote kiasi kwamba mitaji inakata. so wameamua kurudi en...
Sunday, 19 May 2013
Saturday, 18 May 2013
HALI YA MIUNDOMBINU NI MBAYA WILAYANI MAKETE
Picha hizi zinaonesha maeneo mbalimbali ya barabara wilayani Makete mkoani Njombe ambazo zimeharibika kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha wilayani humo, kwa hivi sasa mvua zimemalizika tunaomba wahusika waanze kuzifanyia ukarabaiti(Picha na msumari bloggers)
IFAHAMU SERA YA GESI TANZANIA AMBAYO WABUNGE WALIELEKEZWA
Draft 3- The Natural Gas Policy of Tanzania -2013(Rasimu ya Sera ya Gesi Asilia)
Nimepata muda kidogo wa kuipitia hii rasimu ya 3 nikiwa safarini kwenda Tabora kwa shughuli za chama changu cha CHADEMA , nina maoni ya awali kama ifuatavyo;
1). Kwa ujumla kupata Sera mpya ya gesi asilia ni hatua muafaka japo imechelewa sana. Hata hivyo ni bora kuchelewa kuliko kutofika kabisa. Ni vema wananchi wachukue fursa hii kuisoma na kuijadili rasimu hii na kuiboresha ili iwezeshe wananchi wenyewe kufaidika na utajiri ambao nchi yetu imejaaliwa.
2). Sera ina jumla ya sura Sita. Sura ya kwanza ya inaweka sababu na masuala ya jumla na utangulizi . Sura ya pili inaweka sababu za kuwepo kwa sera mpya na madhumuni maalumu, Sura ya tatu ndio yenye matamko ya msingi ya kisera (fundamental policy issues) ikiwemo masuala ya miundombinu ya gesi kwa ajili ya soko la ndani, usimamizi wa mapato yatokanayo na gesi asilia na masuala ya ‘’ local content’’. Sura hii pia imezungumzia masuala ya uwazi na uwajibikaji. Sura ya nne ni masuala ya mfumo wa kisheria na udhibiti na sura ya tano ni taasisi za usimamizi wa sera ya gesi asilia. Sura ya sita ni hitimisho. Kila sura imeweka matamko ya kisera.
3). Rasimu ya sera imeshindwa kutofautisha suala la Mafuta na Gesi kuwa ni suala la Muungano au sio suala la muungano katika muktadha wa Katiba mpya inayojadiliwa sasa. Hii inadhihirisha umuhimu wa kuwianisha mchakato wa katiba na michakato mingine inayoendelea nchini. Hivi sasa Zanzibar inajiandaa kuwa na sera na sheria yao ya mafuta ya gesi, iweje sera hii itamke gesi asilia ni mali ya Jamhuri ya Muungano wakati upande mmoja wa Muungano utakuwa unafaidi utajiri wake peke yake? Rasimu ya sera imeshindwa kutambua kuwa kuna vitalu vya mafuta na gesi ya (vitalu namba 9-12) vimesimamisha shughuli kwa sababu Serikali ya Zanziabar haitambui mafuta na gesi kuwa suala la muungano. Rasimu inapaswa kuzingatia jambo hili kabla ya kupata sera yenyewe.
4). Rasimu imetamka katika ukurasa wa 9 kwamba sera hii haitambui shughuli za utafutaji (‘This policy document only covers mid-and downstream segments’ ndio nukuu ya neno kwa neon ya Sera hii). Hiki ni kichekesho cha milenia .
Taifa linawezaje kuandika sera ya gesi asilia kwa upande wa uchuuzi tu (biashara) na kuacha kazi yenyewe haswa ya utafutaji na uchimbaji (exploration and exploitation are upstream). Shughuli za utafutaji na uchimbaji ndio msingi haswa wa sera ya gesi asilia.
Mikataba yote huamuliwa kwa kuzingatia kwanza utafutaji, shughuli nyingine ni biashara tu ya kitakachogunduliwa . Rasimu kuacha kabisa eneo la utafutaji na uendelezaji (upstream) ni sawa na kutokuwa na sera kabisa.
Kwa namna eneo hili lilivyoachwa kuna harufu ya mkakati wa siri wa kuwanyima wananchi msimamo wa kisera kuhusu utajiri wao unavyonyonywa . Sentensi hii yenye maneno 10 katika uk. wa 9 wa kijitabu cha rasimu ya sera unaondoa kabisa umuhimu wa sera yenyewe wakati dhumuni kuu la sera linatamkwa uk.6 kwamba Gesi asilia ni mali ya wananchi wa ‘Jamhuri ya Muungano’ wa Tanzania’’ kurasa tatu baadaye zinaiondoa sera kwenye eneo hilo la umiliki wa mali hii ( Upstream). Tumeamua kuandika sera ya uchuuzi wa gesi asilia?
5). Rasimu katika 3.2.2(uk.24) imeweka matamko ya kisera kuhusu uwazi na uwajibikaji . Uwazi ndio eneo ambalo watanzania wengi walikuwa wanasubiri kwa hamu sana . Usiri wa mikataba katika sekta mbali mbali nchini ni chanzo cha ufisadi na uporaji wa utajiri wa mali yetu. Sera hii imeJibu swala hili? HAPANA. Sera haisemi ni namna gani mikataba itakuwa wazi kwa wananchi. Sera haisemi ni namna gani wananchi wataiwajibisha Serikali na vyombo vyake (Accountability) kwenye masuala ya mafuta na gesi. Sera imepiga porojo kuhusu uwazi na uwajibikaji. Bila misingi imara ya Uwazi na Uwajibikaji katika rasilimali ya gesi asilia, sera haina maana yoyote ile.
6). Serikali ni lazima ijue kwamba hivi sasa nchi yetu nchi tajiri yenye watu masikini.[i] sera ya gesi inapaswa kutuondoa kuwa nchi yenye laana ya rasilimali. Sera hii haina mwelekeo huo kabisa . Sera inapaswa kuwezesha wananchi kupata thamani ya maliasili yetu na kuwezesha matumizi mazuri ya mapato yatokanayo na utajiri wa nchi.
Sera yetu lazima ioneshe dhahiri kwamba gesi asilia ni mali ya wananchi na uendelezaji na unyonyaji wa rasilimali hii utafaidisha wananchi kwanza na kwa ruhusa yao (Prior informed Consent Principle) sera ni lazima itamke hilo kinagaubaga.Sera ni lazima ionyeshe kuwa katika ushindani wa soko makampuni ya mafuta na gesi asilia yatapata faida ya halali ( normal retuns) ya uwekezaji wao na kwamba lolote linalozidi litabakia kuwa mali ya wananchi wa Tanzania.
Mkakati wa makampuni ya mafuta na gesi asilia ni kuhakikisha taifa linapata kiduchu na wanasaidia serikali kutoa majibu ya kipato hicho kiduchu. Watanzania hawatakubali tena.
7). Ni lazima tuseme kuwa tunataka utajiri wetu uwe neema kwa wananchi wetu, na siyo laana. Maendeleo yetu yatategemea ni namna gani tunafaidika na utajiri wetu wa maliasili kama gesi asilia. Sera ya Gesi Asilia itujengee imani hiyo. Hii Sera (Rasimu) inapaswa iangaliwe upya na hasa maeneo ya uwazi na uwajibikaji.
Kabwe Z. Zitto, Mb Kigoma Kaskazini
Tabora, tarehe 18 Mei 2013

HAWA NDIYO WATAKAOONGOZA KAMPENI ZA UDIWANI ARUSHA KUPITIA CHADEMA
Kata
ya Kimandolu itaongozwa na Dr Slaa,Mh Sugu,Mh Nassari, na Alphonce
Mawazo. Kata ya Themi itaongozwa na Mh Msigwa, Mh Zitto, Mh Lucy
Owenya,na Mh Parresso, Kata ya Elerai itaongozwa na Mh Lema, Mh Mnyika,
Mh Halima Mdee na Mh Rosse Kamili, Kata ya Kaloleni atakuwepo Mh Mbowe,
Kamanda mkuu, Tundu Antipas Lissu, Mabere Nyaucho Marandu, na Mh Natse,
Leo uzinduzi wa kata zote nne utafanyika viwanja vya Ngarenaro,Kamanda
Mbowe atazindua kwa kutumia Chopa
TUNDU LISU AZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA ISEKE-SINGIDA, 17.5.2013
Kamanda Lisu ameongozana na Makamanda Hamedi na wenzake leo katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa diwani kata ya Iseke ,jimboni Singida Magharibi . Katika kuelekea kutimia kwa kauli ya Mjinga akijitambua,mwelevu yuko matatani mwenyekiti wa kijiji cha Msambu kupitia CCM amejivua gamba na kujiunga na jeshi la ukombozi . Kata hii ya Iseke ina undwa na vijiji 3 ambavyo ni Iseke, Nkhoiree na Unyangwe . Kamanda anae peperusha bendera ya CHADEMA anaitwa Emmanuel Jackson . Kwa hamasa iliyopo ushindi ni asubuh na mapema
MBUNGE WA CHADEMA AUGUA GHAFLA
MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mwanamrisho Taratibu Abama leo asubuhi aliugua ghafla katika viwanja vya Bunge na kukimbizwa hospitali. Tukio hilo lilitokea wakati akienda kuhudhuria semina ya wabunge kuhusu Rasimu ya Sera ya Gesi Asilia kabla ya kukosa nguvu na kusaidiwa na wenzake kumkimbiza kwenye zahanati ya Bunge.Baada ya kupatiwa huduma ya kwanza bungeni, gari la wagonjwa lilimkimbiza Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) ambako amelazwa.
Kwa mujibu wa waliomshuhudia, alianza kuishiwa nguvu hali ambayo waliokuwa karibu walimsaidia kumpeleka kwenye zahanati ambako alitundikiwa dripu kabla ya kupelekwa hospitalini. Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Dodoma, Zainabu Chaula alikiri kumpokea mbunge huyo
CHADEMA WAFUNIKA KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO ARUSHA
MAMIA YA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA WAKIWA KATIKA MKUTANO WA UZINDUZI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI.
Subscribe to:
Posts (Atom)