Popular Posts

Wednesday, 12 June 2013

MULUGO ANASWA AKITOA RUSHWA




     CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemfikisha Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillip Mulugo, mbele ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za kutoa rushwa ya ahadi ya mifuko ya saruji na fedha taslimu 40,000 kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi. Chama hicho pia kimemfungulia faili la tuhuma za ubakaji mgombea udiwani wa Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mdogo wa kata ya Mbalamaziwa, Zuberi Nyomolela, kwa kosa kuishi kinyumba na binti mwanafunzi. Hayo yamesemwa jana katika kijiji cha Mbalamaziwa na mwanasheria wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Sinkara Lucas, kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Mbalamaziwa, uliohudhuriwa na mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe.

      “Ndugu zangu wakati wa kampeni hasa za nyumba kwa nyumba tulikuwa tunakutana na maneno maneno hivi yanazungumzwa kuhusu mgombea wa CCM, maneno mazito sana, sasa kama kawaida ya CHADEMA kama mnavyojua huwa hatukurupuki, tunafanyia kwanza vitu utafiti kabla hatujatoka hadharani kutuhumu; tunakuwa na ushahidi wa kutosha. “Wananchi wa Mbalamaziwa ninyi ni mashahidi; majuzi alipita hapa Phillip Mulugo akatoa rushwa ya ahadi ya mifuko 20 ya saruji na fedha taslimu 40,000 eti kwa vijana wakanunue mipira lakini wamchague Zuberi...amefanya yote hayo hadharani hapa jukwaani, kinyume cha sheria za uchaguzi na sheria za nchi. Sasa tunao ushahidi na tumeupeleka TAKUKURU na hivi sasa wanalifanyia kazi faili hilo. Wakati wowote atakamatwa

No comments:

Post a Comment