KIKAO CHA WALIMU WA MKOA WA MBEYA CHA
KUJADILI MASLAHI YA WALIMU WA TANZANIA-Tarehe 3 August, 2013.
1.
CHAMA CHA WALIMU-CWT NA WALIMU.
a. Umuhimu wa chama cha walimu katika
kufuatilia maslahi na madai mbalimbali ya walimu. CWT imeshindwa kuwasaidia
walimu katika kufuatilia madai ya maslahi mbalimbali kama vile kupanda
madaraja, malimbikizo ya mishahara, nauli n.k ambapo jukumu la chama sasa
jukumu hili limekuwa likifanywa na walimu wenyewe alihali tukichangia chama kwa
ajili ya kutetea walimu.
b. Uwajibikaji wa Chama cha walimu-CWT
kwa walimu. CWT imeshindwa:-
i.
Kutoa,
elimu, taarifa, mbalimbali kwa walimu hii ikiwemo katiba ya Chama Cha
Walimu-CWT, Kanuni za kudumu utumishi wa umma kwa walimu ili kutufanya tutambue vizuri haki na wajibu
wetu kama watumishi.
ii.
Kutoa
taarifa kwa walimu juu ya mwenendo wa majadiliano kati ya serikali na CWT
kuhusu madai ya nyongeza ya mishahara kwa 100%, posho ya mazingira magumu,
posho ya kufundishia na posho ya walimu wa sayansi n.k. CWT imekaa kimya kwa
muda sasa tangu mahakama isitishe mgomo wetu na kutuamuru turudi kazini huku
mahakama ikiiamuru serikali kukaa meza moja na CWT ili kufikia muafaka. Umepita
muda sasa chama cha Walimu-CWT hakijatoa taarifa yoyote kwa walimu kuhusu hatma
ya madai hayo ya walimu. Hii inadhihirisha kuwa chama cha walimu aidha kimeamua
kuwasaliti walimu kwa kushirikiana na serikali yaani mwajiri wetu.
c. MCHANGO wa kila mwezi. Walimu wa mkoa
wa Mbeya kwa niaba ya walimu wa Tanzania tunahoji uhalali wa chama cha
walimu-CWT kukata fedha kila mwezi kama mchango wa chama alihali si wanachama
wa Chama hicho.
2. SERIKALI YA JAMHURI MUUNGANO WA TANZANIA NA WALIMU
Serikali
ya jamhuri ya muungano wa Tanzania imekuwa ikifanya yafuatayo kwa kwa kada ya
utumishi wa umma hasa ualimu:-
a. Kuligawa Taifa kimakundi na kuvunja umoja
wa kitaifa kwa kufanya yafuatayo:-
i.
Kuweka
tofauti kubwa ya kipato cha mshahara kwa wafanyakazi wa serikali wenye elimu
sawa katika kada tofauti. Mfano kwa mujibu wa waraka wa watumishi wa serikali
Na 1. Wa mwaka 2013, wenye Kumb. Na. CAC.205/228/01/C/14 wa Julai 2, 2013
uliosainiwa na Katibu mkuu Utumishi Ndugu George D. Yambeshi. Unaoonyesha
marekebisho ya mishahara kwa watumishi wa serikali. Katika waraka huu
unaendelea kudidimiza kada ya ualimu kulingana na kada zingine kama vile kada
ya afya, sheria na kilimo na utafiti ambapo kada hizi hulipwa mishahara mikubwa
kuliko ya walimu. Kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977 Toleo la mwaka 2005 ibara ya 23(1) inasema “Kila Mtu, bila ya kuwapo ubaguzi
wa aina yoyote, anayo haki ya kupata ujira unaolingana na kazi yake, na watu
wote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao watapata malipo kulingana na uwezo
na kiasi kiasi na sifa za kazi wanazozifanya”. Je, serikali ya Jamhuri
ya Muungano inatulipa walimu ikitofautisha mshahara huo na kada zingine kwa
vigezo kwamba:-
a. Uwezo wetu wa kufanya ya kazi
haufanani na kada hizo?
b. Umuhimu wa kada ya ualimu ni mdogo
tofauti na kada hizo nyingine?
c. Sifa za kielimu walizonazo walimu ni
tofauti kabisa na kada hizo?
d. Umuhimu wa walimu na elimu ni mdogo
katika Jamhuri yetu ya Muungano wa Tanzania ukilinganisha na sekta kama vile
Kilimo na Afya?
e. Au hii ni mbinu ya “divide and rule”
kwa wafanyakazi?
NGAZI YA
ELIMU
|
UALIMU/ ELIMU
|
KILIMO
|
AFYA
|
Certificate (Cheti)
|
Tsh 344,000/=
|
Tsh 1,060,000/=
|
Tsh 562,000/=
|
Diploma (Stashahada)
|
Tsh 432,500/=
|
Tsh 1,252,000/=
|
Tsh 821,000/=
|
Degree (Shahada)
|
Tsh 589,000/=
|
Tsh 1,473,000/=
|
Tsh 994,000/=
|
Jedwali
hili ni kwa mujibu wa waraka huo uliotajwa hapo juu
|
|||
b. Kulubuni vyama vya wafanyakazi
ikiwemo Chama cha Walimu-CWT ili kuacha majukumu yake ya kutetea na kutoa elimu
juu ya haki na wajibu wa wafanyakazi ila vyama hivyo kushirikiana na serikali
kukandamiza haki za wafanyakazi. Baadhi ya mbinu ambazo serikali imekuwa
ikizitumia ni kama vile:- Moja, kuwapatia posho kubwa wakilishi na viongozi wa
vyama pindi serikali na wawakilishi hawa wanapo kutana katika kujadili maslahi
ya wafanyakazi ili kuwaziba mdomo. Pili, Kuwatishia kusitisha utaratibu wa
kukusanya michango ya wanachama ila vyama vyenyewe vikusanye kwa njia wanaoijua
wao. Tatu, kutofanya ukaguzi wa mara kwa mara katika vyama hivi vya wafanyakazi
katika mapato, matumizi na miradi mbalimbali. Hii inasababisha vyama vya
wafanyakazi kutofanya kazi ya kutetea wafanyakazi bali kutumia fedha na mali za
vyama kwa manufaa binafsi.
c. Kutumia vitisho na kauli za kutisha
kudidimiza maslahi na haki za watumishi wa umma ikiwemo walimu. Viongozi wa
serikali kama mawaziri na viongozi wengine waandamizi wa serikali wamekuwa
wakitumia vitisho kwa wafanyakazi kama njia ya kuwanyamazisha wasidai maslahi
yao.
3. TAMKO KWA CHAMA CHA WALIMU-CWT NA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA.
Sisi Walimu wa Mkoa wa Mbeya tunatoa
siku 30 kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Na Chama Cha
Walimu-CWT, Kuanzia leo Tarehe 03 August, 2013 hadi Tarehe 03 September, 2013
itekeleze yafuatayo:-
I.
CHAMA CHA WALIMU-CWT
·
Kutoa taarifa ya fedha ya (Makusanyo
ya kila mwezi) na mapato na matumizi ya chama hicho kwa walimu.
·
Kutoa taarifa ya wapi wamefikia
kuhusu madai yetu dhidi ya serikali ya nyongeza ya mishahara kwa 100% na posho
za mazingira magumu na kufundishia n.k, kwani ni muda sasa walimu tumechoka na
ukimya wa CWT juu ya suala hilo.
·
Chama kisitishe makato haraka kwa
walimu ambao si wanachama wa chama hicho.
·
Mkaguzi mkuu wa serikali (CAG) akague
mwenendo wa miradi, mapato na matumizi ya Chama Cha Walimu-CWT na kutoa Taarifa
kwa Walimu.
·
Kuboresha mfumo wa mawasiliano kutoka
viongozi wajuu wa chama hadi walimu katika ngazi ya tawi.
II.
SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
·
Serikali iweke sawa uwiano wa
mishahara kisekta kulingana na viwango vya elimu kwa watumishi wa umma.
·
Serikali isitishe vitisho na matamko
yenye vitisho kwa watumishi wa umma.
·
Serikali ipunguze kiwango cha kodi
kubwa na kandamizi kwa watumishi wa umma, na itafute vyanzo vingine vya mapato
·
Serikali isizue watumishi kujiendeleza
kwa sababu yoyote ile ili mradi wawewamekidhi vigezo vya kisheria vya
kujiendeleza.
·
Serikali isitishe mpango wa kuligawa
taifa kwa misingi ya maslahi binafsi, Kielimu, Kisekta na Nyadhifa.
·
Serikali ipandishe madaraja walimu
waliojiendeleza kielimu ili kuwapa motisha.
Imetolewa na Walimu Wa
Mkoa Wa Mbeya-Tarehe 03 August, 2013- Mkoani Mbeya.