Popular Posts

Saturday, 3 August 2013

HILI NDO TAMKO LA WALIMU WA MKOA WA MBEYA JUU YA KUPANDA KWA MISHAHARA, July 2013

Tamko hili limetolewa leo tarehe 3 august 2013, mkoani mbeya katika ukumbi wa royal zambezi

KIKAO CHA WALIMU WA MKOA WA MBEYA CHA KUJADILI MASLAHI YA WALIMU WA TANZANIA-Tarehe 3 August, 2013.


1.     CHAMA CHA WALIMU-CWT NA WALIMU.
a.      Umuhimu wa chama cha walimu katika kufuatilia maslahi na madai mbalimbali ya walimu. CWT imeshindwa kuwasaidia walimu katika kufuatilia madai ya maslahi mbalimbali kama vile kupanda madaraja, malimbikizo ya mishahara, nauli n.k ambapo jukumu la chama sasa jukumu hili limekuwa likifanywa na walimu wenyewe alihali tukichangia chama kwa ajili ya kutetea walimu.
b.      Uwajibikaji wa Chama cha walimu-CWT kwa walimu. CWT imeshindwa:-
i.                    Kutoa, elimu, taarifa, mbalimbali kwa walimu hii ikiwemo katiba ya Chama Cha Walimu-CWT, Kanuni za kudumu utumishi wa umma kwa walimu  ili kutufanya tutambue vizuri haki na wajibu wetu kama watumishi.
ii.                  Kutoa taarifa kwa walimu juu ya mwenendo wa majadiliano kati ya serikali na CWT kuhusu madai ya nyongeza ya mishahara kwa 100%, posho ya mazingira magumu, posho ya kufundishia na posho ya walimu wa sayansi n.k. CWT imekaa kimya kwa muda sasa tangu mahakama isitishe mgomo wetu na kutuamuru turudi kazini huku mahakama ikiiamuru serikali kukaa meza moja na CWT ili kufikia muafaka. Umepita muda sasa chama cha Walimu-CWT hakijatoa taarifa yoyote kwa walimu kuhusu hatma ya madai hayo ya walimu. Hii inadhihirisha kuwa chama cha walimu aidha kimeamua kuwasaliti walimu kwa kushirikiana na serikali yaani mwajiri wetu.
c.       MCHANGO wa kila mwezi. Walimu wa mkoa wa Mbeya kwa niaba ya walimu wa Tanzania tunahoji uhalali wa chama cha walimu-CWT kukata fedha kila mwezi kama mchango wa chama alihali si wanachama wa Chama hicho.

2.     SERIKALI YA JAMHURI MUUNGANO WA TANZANIA NA WALIMU
Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania imekuwa ikifanya yafuatayo kwa kwa kada ya utumishi wa umma hasa ualimu:-
a.      Kuligawa Taifa kimakundi na kuvunja umoja wa kitaifa kwa kufanya yafuatayo:-
i.                    Kuweka tofauti kubwa ya kipato cha mshahara kwa wafanyakazi wa serikali wenye elimu sawa katika kada tofauti. Mfano kwa mujibu wa waraka wa watumishi wa serikali Na 1.  Wa mwaka 2013, wenye Kumb. Na. CAC.205/228/01/C/14 wa Julai 2, 2013 uliosainiwa na Katibu mkuu Utumishi Ndugu George D. Yambeshi. Unaoonyesha marekebisho ya mishahara kwa watumishi wa serikali. Katika waraka huu unaendelea kudidimiza kada ya ualimu kulingana na kada zingine kama vile kada ya afya, sheria na kilimo na utafiti ambapo kada hizi hulipwa mishahara mikubwa kuliko ya walimu. Kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Toleo la mwaka 2005 ibara ya 23(1) inasema “Kila Mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa aina yoyote, anayo haki ya kupata ujira unaolingana na kazi yake, na watu wote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao watapata malipo kulingana na uwezo na kiasi kiasi na sifa za kazi wanazozifanya”. Je, serikali ya Jamhuri ya Muungano inatulipa walimu ikitofautisha mshahara huo na kada zingine kwa vigezo kwamba:-
a.      Uwezo wetu wa kufanya ya kazi haufanani na kada hizo?
b.      Umuhimu wa kada ya ualimu ni mdogo tofauti na kada hizo nyingine?
c.       Sifa za kielimu walizonazo walimu ni tofauti kabisa na kada hizo?
d.      Umuhimu wa walimu na elimu ni mdogo katika Jamhuri yetu ya Muungano wa Tanzania ukilinganisha na sekta kama vile Kilimo na Afya?
e.      Au hii ni mbinu ya “divide and rule” kwa wafanyakazi?
 NGAZI YA ELIMU
UALIMU/ ELIMU
KILIMO
AFYA
Certificate (Cheti)
Tsh 344,000/=
Tsh 1,060,000/=
Tsh 562,000/=
Diploma (Stashahada)
Tsh 432,500/=
Tsh 1,252,000/=
Tsh 821,000/=
Degree (Shahada)
Tsh 589,000/=
Tsh 1,473,000/=
Tsh 994,000/=
Jedwali hili ni kwa mujibu wa waraka huo uliotajwa hapo juu

b.      Kulubuni vyama vya wafanyakazi ikiwemo Chama cha Walimu-CWT ili kuacha majukumu yake ya kutetea na kutoa elimu juu ya haki na wajibu wa wafanyakazi ila vyama hivyo kushirikiana na serikali kukandamiza haki za wafanyakazi. Baadhi ya mbinu ambazo serikali imekuwa ikizitumia ni kama vile:- Moja, kuwapatia posho kubwa wakilishi na viongozi wa vyama pindi serikali na wawakilishi hawa wanapo kutana katika kujadili maslahi ya wafanyakazi ili kuwaziba mdomo. Pili, Kuwatishia kusitisha utaratibu wa kukusanya michango ya wanachama ila vyama vyenyewe vikusanye kwa njia wanaoijua wao. Tatu, kutofanya ukaguzi wa mara kwa mara katika vyama hivi vya wafanyakazi katika mapato, matumizi na miradi mbalimbali. Hii inasababisha vyama vya wafanyakazi kutofanya kazi ya kutetea wafanyakazi bali kutumia fedha na mali za vyama kwa manufaa binafsi.
c.       Kutumia vitisho na kauli za kutisha kudidimiza maslahi na haki za watumishi wa umma ikiwemo walimu. Viongozi wa serikali kama mawaziri na viongozi wengine waandamizi wa serikali wamekuwa wakitumia vitisho kwa wafanyakazi kama njia ya kuwanyamazisha wasidai maslahi yao.
3.      TAMKO KWA CHAMA CHA WALIMU-CWT NA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Sisi Walimu wa Mkoa wa Mbeya tunatoa siku 30 kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Na Chama Cha Walimu-CWT, Kuanzia leo Tarehe 03 August, 2013 hadi Tarehe 03 September, 2013 itekeleze yafuatayo:-
I.                   CHAMA CHA WALIMU-CWT
·         Kutoa taarifa ya fedha ya (Makusanyo ya kila mwezi) na mapato na matumizi ya chama hicho kwa walimu.
·         Kutoa taarifa ya wapi wamefikia kuhusu madai yetu dhidi ya serikali ya nyongeza ya mishahara kwa 100% na posho za mazingira magumu na kufundishia n.k, kwani ni muda sasa walimu tumechoka na ukimya wa CWT juu ya suala hilo.
·         Chama kisitishe makato haraka kwa walimu ambao si wanachama wa chama hicho.
·         Mkaguzi mkuu wa serikali (CAG) akague mwenendo wa miradi, mapato na matumizi ya Chama Cha Walimu-CWT na kutoa Taarifa kwa Walimu.
·         Kuboresha mfumo wa mawasiliano kutoka viongozi wajuu wa chama hadi walimu katika ngazi ya tawi.
II.                 SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
·         Serikali iweke sawa uwiano wa mishahara kisekta kulingana na viwango vya elimu kwa watumishi wa umma.
·         Serikali isitishe vitisho na matamko yenye vitisho kwa watumishi wa umma.
·         Serikali ipunguze kiwango cha kodi kubwa na kandamizi kwa watumishi wa umma, na itafute vyanzo vingine vya mapato
·         Serikali isizue watumishi kujiendeleza kwa sababu yoyote ile ili mradi wawewamekidhi vigezo vya kisheria vya kujiendeleza.
·         Serikali isitishe mpango wa kuligawa taifa kwa misingi ya maslahi binafsi, Kielimu, Kisekta na Nyadhifa.
·         Serikali ipandishe madaraja walimu waliojiendeleza kielimu ili kuwapa motisha.
Imetolewa na Walimu Wa Mkoa Wa Mbeya-Tarehe 03 August, 2013- Mkoani Mbeya.

Tuesday, 23 July 2013

MISHAHARA MIPYA NI JANGA KWA WALIMU



Kutokana na barua yenye Kumb Na CAC.205/228/01/C/14 ya tarehe 2 Julai,2013, Kutoka Menejiment ya utumishi wa umma, inayohusu kupandisha mshahara kwa watumishi wa serikali yenye kichwa cha habari “WARAKA WA WATUMISHI WA SERIKALI NA. 1 WA MWAKA 2013, MAREEKEBISHO YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA SERIKALI” Inasema Serikali inaendelea kutekeleza sera ya malipo ya mishahara na motisha katika utumishi wa umma mwaka 2010. Katika hatua za kutimiza malengo ya sera hii, serikali inafanya marekebisho ya mishahara ya watumishi wake kuanzia tarehe 1 julai, 2013. Kutokana na marekebishi hayo kima cha chini kitakuwa kutoka 170,000/= hadi tsh 240,000/= kwa mwezi. Mishahara ya watumishi wengine imeongezwa kwa wastani wa 8.41% . imesainiwa na KATIBU MKUU (UTUMISHI G.D.Yambeshi)(Mwisho wa kunukuu).
                Barua hiyo ambayo inaonekana kuwa mwiba kwa watumishi wa kada ya UALIMU ambao walidhani serikali itajibu madai yao ya nyongeza ya mishahara, subira hiyo haijazaa matumaini kwani kwa mujibu wa waraka huo kada ya ualimu inaonekana iko nyuma ya kada za afya na kilimo. Hii ni sehemu ya waraka huo ukianisha madaraja ya mishahara mipya kuanzia julai 1, 2013.(N:B Kwa wale wasiojua ngazi ya mshahara ya B ni ya mwenye cheti (certificate), C= Diploma, D= Degree)
                WALIMU
TGTS B1=  344,000/=
TGTS C1= 432,500/=
TGTS D1= 589,000/=
TGTS E= 769,000/=
TGTS F= 1,003,000/=
TGTS G= 1,320,000/=
Wakati kwa kada ya KILIMO mambo ni mazuri kabisa kama ifuatavyo
B= 1,060,000/=
C=1,252,000/=
D= 1,473,000/=
E=1,736,000/=
POLENI SANA WALIMU KWA KUENDELEA KUNYONYWA HAKI ZENU.
Katika waraka huu sehemu ya mwisho unasema
WARAKA HUU NI KUMBUKUMBU NA TAARIFA YA SERIKALI NA HAIRUHUSIWI KUTANGAZWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI

Monday, 17 June 2013

SOMA UNYAMA WALIOTENDEWA WAFUASI NA VIONGOZI WA CHADEMA NA WAFUASI WAO KATIKA UCHAGUZI MDOGO



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatoa taarifa za Hujuma zinazoendelea katika chaguzi za marudio kwa kata mbalimbali hapa nchini.
Kwa masikitiko makubwa CHADEMA kinatoa taarifa ya matukio ya kusikitisha yanayoendelea katika chaguzi hizi,kama ifuatavyo;

1. KATA YA IYELA,MBEYA.
Katika kata hii Gari la Chama Cha Mapinduzi lenye Usajili namba T 704 BEU,likiwa na watu wawili wanaotambulika kwa majina ya Moris na Nosy,waliwateka vijana wa CHADEMA na mmoja wao kuchomwa kisu,aliechomwa kisu anaitwa Meshack Bernard.Vijana wa CCM waliokamatwa wameachiwa huru na jeshi la polisi na sasa wanatumia gari nyingine yenye rangi nyekundu Toyata Surf namba T-173 ANE,wakiendelea kufanya vitendo hivo viovu.

Na katika kituo cha kupigia kura cha SIDO ,vituo 3 vimelundikwa sehemu moja na eneo hilo kuna Karakana ambayo inawafanya watu kuingia na kutoka kinyume na sheria za uchaguzi.

2. KATA YA MBALAMAZIWA ,MUFINDI KASKAZINI.

Watu sita wamepigwa kwa marungu na visu na kuumizwa vibaya muda huu.Idadi ya vitisho katika kata hii ni kubwa mno hali iliyopelekea idadi ndogo ya watu kujitokeza kupiga kura.

4. NYAMPU LUKANO, SENGEREMA 

Viongozi na makada wa CCM waligawa mapanga kwa vijana wao na kukata watu.Vijana 3 wa CHADEMA wamechomwa kisu na kujeruhiwa vibaya sana.

5:KATA YA MINEPA,MOROGORO.

Tukio lililotokea huko ni kuchomwa moto PIKIPIKI mali ya Chama(M4C) na vijana wa CCM(greenguard). Vile vile Katibu wa Chama wilaya ndugu Lucas Daniel amepigwa na kuumizwa na mwenzake amekatwa vidole.

3.KATA YA MANCHIRA,SERENGETI-MARA
Tumepokea taarifa kuwa Mkuu wa Wilaya kujihusisha na vitendo vya utoaji rushwa kwa wapiga kura,kwa lengo la kuwezesha CCM kushinda. Vijana wetu ni mashuhuda wa tukio hilo na wako tayari kutoa ushahidi juu ya hili piai wameshuhudia vijana wa CCM wakiwa na Bastola na baadhi yao kukamatwa na vijana wa CHADEMA na kupelekwa polisi

Hali kadhalika Jeshi la Polisi limekamata vijana wetu kuanzia jana jioni hadi leo hii na wamekuwa wakitumia mabomu na hivyo kuwajeruhi.Kuna vijana ambao wametekwa na hawajulikani walipo na majina yao na wanakotoka ni kama ifuatavyo
-Barena Maro-Bwitengi
-Samson Ogao-Rwamchanga
-Adam Samson-Bwitengi
-Emmanuel Eliya-Bwitengi
-Onyango Otaro-Miseke
-Manginare Samson-Miseke
-Elija Wilson-Miseke
-Banage Nanai-Rwamchanga
-Matororo saina-Rwamchanga
-Pikipiki Simba-Rwamchanga
John Oninga-Rwamchanga

Na baadhi ya gari zifuatazo zilikua zikishiriki opereshani ya kuwateka wafuasi wa CHADEMA magari hayo ni yenye namba zifuatazo za usajili T286 BFB, T545BFE zote Landcruiser za CCM na T352 AHD.
Diwani wa CHADEMA kata ya MUGUMU Mh.Marwa Waryoba amekamatwa na polisi yupo kituoni ili kumyima fursa ya kukugua zoezi la upigaji kura kama sheria inavyomtaka.

3. KATA YA MIANZINI,DAR ES SALAAM.

Tukio lililotokea huko ni kutekwa kwa wanachama na kiongozi wa Chama. Watu hawa walitekwa na kufungwa vitambaa vyeusi machoni,kisha kupigwa na kuumizwa vibaya. Mmoja kati ya vijana hao ni Katibu wa Vijana CHADEMA tawi la machinjioni anaeitwa Julius Vedastua na mpaka sasa yuko hospital.
Tukio lingine linaloendelea katika kata hii ni vitendo vya Rushwa,makada wa CCM wamekuwa wakivuta watu kutoka kwenye mistari na kuwapatia pesa.
Hali kadhalika kwa baadhi ya maeneo katika kata hii ni kuwa na wasimamizi wengi katika kituo kimoja,na wasimamizi hao wamekuwa wakiwaongoza watu kupiga kura mpaka kwenye ile sehemu ya kupigia kura na kuwapa maelezo juu ya nani wa kumchagua,kitendo ambacho ni kinyume na Sheria.

KATA YA STESHENI, NACHINGEA,LINDI.
Taarifa tulizonazo zinasema kuwa Magari ya CCM yamekuwa yakisomba wapiga kura na kati ya magari yanayotumika ni gari lenye usajili namba T670 DEU.

KATA YA DONGOBESH,MANYARA.
Katika kata hiyo,makada wa CCM wanawavamia katika vilabu vya pombe na kuwanunulia wananchi pombe kama hongo ya kutaka kupigiwa kura,na baada ya kuwanunulia pombe wamekuwa wakiwasomba kwa magari na kuwapeleka katika vituo vyao vya kupigia kura,kitendo hichi ambacho ni kinyume na sheria.

KATA YA GENGE,TANGA.
Matukio yaliyotokea huko ni vijana wa CCM kuwakamata vijana wetu wa Red Brigade na kuwapiga na kuwaumiza. Tukio hili limesharipotiwa polisi.

KATA YA MAKUYUNI,ARUSHA.

Vijana wa Kimasai ambao wamekodiwa na Chama cha Mapinduzi wamekuwa wakivamia wanachama na viongozi wetu na kuwapiga,katika kata hii ndio tukio la kumpiga na kumjeruhi Mh Mbunge Joshua Nasari limefanyika.

Aidha kuhusu mauaji ya Arusha Mwenyekiti wa Chama Taifa,Mh Freeman Mbowe ameshatoa


msimamo wa chama juu ya tukio hilo.


Imetolewa na :

Erasto Tumbo(Afisa Mwandamizi Uenezi)

Thursday, 13 June 2013

MSANII LANGA AFARIKI DUNIA, PIGO LINGINE KWA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA



Langa Kileo (msanii wa Hip Hop Tanzania, pichani) amefariki dunia leo hii.
Langa alipelekwa hospitali akiwa hajitambui. Anadaiwa kuwa alikumbwa na Malaria kali sana, Hali iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Muhimbili jana.
Uchunguzi wa chanzo cha kifo chake bado unaendelea.
Msanii Langa aliwahi kutamba na kikundi cha Wakilisha pamoja na witness na sara ni miongoni mwa wasanii wakongwe wa bongo flava nchini Tanzania.
Mungu amrehemu